Mawakili Wapambana Mbele ya Majaji 3, Sabaya Agoma Kuongea Chochote




Rufaa ya kesi ya kupinga maamuzi ya mahkama ya kuu ya kumuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, lengai Ole Sabaya Silvester Nyegu na Daniel Mbura wenzake imeanza kusikilizwa katika mahakama ya rufaa huku upande wa jamhuri ukileta hoja tano kwa nia ya kuishawishi mahakama kuwatia hatiani wajibu rufaa.

Kesi hiyo imeanza kusikilizwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Jacobs Mwambegele akisaidiana na majaji Ignas Kitusi na Leila Mngonya.

Hoja zilizowasilishwa na mawakili wa jamhuri ni pamoja na mahakama kukosea kwa kuwaachia huru washtakiwa ikiwa ni kutokutoa nafasi kwa upande wa jamhuri kumuuliza maswali ya dodoso shahidi wa pili.

Hoja nyingine jaji aliyetoa hukumu ya kuwaachia huru hakujielekeza vizuri katika kuwaachia huru washtakiwa ikiwa ni pamoja na sio ushahidi wa shahidi wa pili pekee ambao ulitumika kuwatia wahstakiwa hatiani bali kulikuwa na ushaidi mwingine.


Kutokana na hoja hizo wameomba jopo la majaji wanaosikiliza rufaa kuwatia hatiani washtakiwa hao kwa kuwa makosa yao ya unyang’anyi wa kutumia silaha yalidhibitika.

Wakili Moses mahuna akiongoza jopo la mawakili wa wajibu rufani amesema hukumu ya rufaa ya kwanza ilikuwa sahihi ikiwemo kipengele cha unyang’anyi wa makundi ambacho kililalamikiwa na uapande wa Jamhuri

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kiongozi wa jopo la majaji Jacobos Mwambegele amesema watakaa na kutafakari nakuandaa uamuzi na pande zote zitajulishwa kupitia ofisi ya Naibu Msajili wa Mahakama Kuu.


Lengai ole sabaya na wenzake wawili walihukumiwa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia kwenye makosa matatu ya unyang’anyi wa kutumia silaha na baadaye walikata rufaaa mahakama kuu na kuachiwa huru.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad