Mbunge akerwa mawaziri ‘kuchati’ bungeni, aomba mwongozo





MBUNGE wa Songwe, Philipo Mulugo, ameomba mwongozo bungeni jijini Dodoma, juu ya tabia ya baadhi ya mawaziri wanaodaiwa kutumia simu (kuchati na kuongea na simu), wakati wabunge wanaendelea kuchangia masuala ya msingi juu ya mustakabali wa nchi.

Mulugo ameomba mwongozo huo Novemba 3, 2023, bungeni jijini Dodoma, wakati Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara anatoa mchango wake kuhusu taarifa za kamati za kudumu za Bunge, juu ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2022.

Mbunge huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amedai wakati Waitara anatoa mchango wake, baadhi ya mawaziri walikuwa wanachati kama anayoyazungumza hayawahusu.

“Mheshimiwa mwenyekiti, kama mbunge wa CCM moyo unaniuma mbunge mwenzetu anapochangia taarifa kama hii, inauma kuona wanaohusika mawaziri wanachati na simu, wanaongea na simu hawajali kile ambacho anakiongea Waitara. Kama vile jambo linapita, haomba mwongozo wako,” amesema Mulugo.

Baada ya Mulugo kutoa ombi hilo, Mwenyekiti wa Bunge, Daniel Sillo, alisema mwongozo kuhusu suala hilo utatolewa baada ya kikao hicho kuisha.

Wakati waitara anachangia, alitaka sheria itungwe ili kuwanyonga watu watakaobainika pasina shaka kuwa ni wezi wa mali za umma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad