Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka EA Radio, Abissay Stephen amesema kuwa, Klanbu ya Simba wanapaswa kuachana na utaratibu wa kufanya maandalizi ya msimu nje ya nchi kwani yanakula pesa na matokeo yake si kama ambavyo mashabiki zao wamekuwa wakitarajia.
Abissay ameongeza kuwa, ni vyema pesa za pre-season Simba wakazitumia kufanya sajili za wachezaji bora wanaowataka ili kuivusha timu hivyo kwenye malengo yake ya msimu husika.
"Msimu huu Simba walikuwa na Pre-season ya mafungu mafungu, nadhani hata wao wenyewe hawakuifurahia sana, kwahiyo wa-concetrate kufanya pre-season ya ndani kwa hoja ya kupata muda mzuri zaidi.
'Kwa hoja ya kupata ukaribu wa kijiografia...kwa hoja kwamba kupunguza gharama, sitaki kuamini kambi ya Tanzania hapa inaweza kuwa milioni 300, kama wakifanya hivyo itawasaidia.
"Yanga wao walifanya pre-season ndani, kwa hiyo walilenga wakaona tupoteza siku nyingi kwenye nchi za watu kusafiri. Kwa hiyo instead (Simba) kupoteza nguvu nyingiii kwenye pre-season na gharama kubwa kama hizo ni heri timu ikae iandae mpango bora wa usajili kupitia hizo fedha, na wapumhuze makali lakini pia wa-concetrate na mazingira ya nyumbani, nadhani hii inaweza ikawalipa.
"Nadhani (Simba) wafanye vitu kwa reasoning nzuri, najua uwezo wa kifedha wanao wa kwenda sehemu yoyote (kufanya pre-season), lakini wasipokuwa wanaangalia vipaumbele vingine, basi wanaweza wakafanya kama fashion, aaah tumetoka labda Brazil eeh wiki moja paap paap.
"Kwa sababu ile huwa naona kuna muda kama inawaongezea msongo wa mawazo hivi, kuna kitu wanatakiwa ku-prove kwamba tumetoka Brazil kwahiyo lazima tu-behave hivi, sasa naona kama inawaongezea kuto-settle, lakini kama wakisema wamebaki hapa vitu vinaenda vizuri tu," amesema Abissay Stephen.