Wachezaji wa Simba walitumia mitandao yao ya kijamii kuomba msamaha Mashabiki na Wapenzi wa timu yao, Matumai ya Wapenzi wa Wekundu wa Msimbazi ni kuona mabadili kwenye uchezaji na matokeo kwa ujumla kitu ambacho hakikutokea.
. 1) Mabadiliko ya Kocha. Simba ilimtimua Kocha mkuu wa timu hiyo Robertinho Oriviera, timu ipo chini ya Kocha wa mpito Daniel Cadena wakati Viongozi Wakitafuta Kocha Mkuu mpya. Cadena anafalsafa zake na aina yake ya mpira anaotaka timu icheze.
Kocha huyu wa mpito hakua na timu kwa muda mrefu hivyo haikua rahisi kwake kubadili kila kitu ndani ya siku chache. Hili limethibitishwa na kikosi kilichoanza siku ya leo, asilimia kubwa ya Wachezaji walioanza leo ni walewale walioanza kwenye mchezo dhidi ya Yanga. Cadena hakupata muda wa kutosha kuambukiza falsafa zake kwa timu ndiyo maana alilazimika kuanza na kikosi kilichoanza na timu kucheza ilivyocheza.
2) Sababu ya pili ni SAIKOLOJIA. Wachezaji wengi wa Simba walizungumzwa sana baada ya mechi ya Yanga, Hawakuzungumzwa kwa mazuri hivyo kama Mchezaji unakua haupo sawa kichwani, hali ya kujiamini inapungua na hali ya kupambana na Ari ya mchezo kwa ujumla inapungua.
Dakika 45 ya kipindi cha kwanza Simba haikucheza vizuri hakukua na ubunifu,upambanaji na Wachezaji hawakuonyesha kuutaka mchezo kwa asilimia 100. Baada ya mabadiliko kidogo timu ilionyesha inapambana lakini hakukua na mpango wa kutafuta magoli kimkakati zaidi ya kupeleka mipira pembeni kwa Mohamed Hussein au Shomari Kapombe Wakapige krosi.
Simba ilihitaji hii mechi kurudisha hali yao ya kiakili vizuri, kwa bahati mbaya ilikutana na moja kati ya timu ngumu yenye Wachezaji wengi wenye uzoefu ya Namungo.Erasto Nyoni, Frank Domayo, Reliant Lusajo, jacob Masawe na wengineo.
Itahitaji muda Simba, kurejea kwenye hali yao ya kawaida na Mwalimu kutengeneza mipango yake jinsi gani atakavyotaka timu yake icheze sambamba na Wachezaji kurudi kwenye utimamu Wao wa kisaikolojia na kujiamini.