"Baada ya tukio hilo mwamuzi alimuonyesha kadi nyekundu mchezaji huyo, ambaye alimfata na kumpiga teke kabla ya kutoka nje," imeeleza taarifa ya Bodi ya Ligi
Pia wachezaji Mudathir Yahya wa Yanga na Feisal Salum (Fei Toto) wa Azam wametozwa faini ya Sh2 milioni kila mmoja kwa kosa la kukataa kupeana mikono na waamuzi na wachezahu kabla ya mechi ya Yanga vs Azam kuanza Oktoba 22 Uwanja wa Mkapa.
Katika taarifa ya Bodi ya Ligi imeeleza wachezaji hao walisimama katika mstari wa kuingia kiwanjani muda wa kupeana mikono kisha kuingia baada ya zoezi hilo kukamilika.
Katika mechi hiyo mwamuzi namba moja, Janeth Balama wa Iringa amesimamishwa mizunguko mitatu kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria za mpira wa miguu.
Mshambuliaji wa Singida Big Stars, Habib Kyombo ametozwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina katika mechi dhidi ya Namungo.
"Mchezaji huyo alionekana akimwaga kimiminika katika goli la Namungo,"
Pia, klabu ya Mashujaa imekumbana na adhabu kama hiyo baada ya mmoja wa viongozi kuonekana akimwaga kimiminika nje ya geti la kuingilia Uwanja wa Mkwakwani Oktoba 25 wakati wakienda kufanya mazoezi.
Mashujaa katika adhabu nyingine imetozwa faini Sh1 milioni kwa kosa la mashabiki wake kurusha chupa kiwanjani baada ya Coastal kupata penalti dakika ya 88.
Bodi ya Ligi Kuu pia imeelezwa kusikitishwa na kitendo cha ukatili na vurugu kilichofanywa na mashabiki waliokuwa wamevaa jezi ya Simba na bluu kumshambukia shabiki wa Yanga katika mechi ya Simba vs Ihefu Uwanja wa Mkapa.
"Bodi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama inakamilisha mchakato wa kuwatambua mashabiki wote waliohusika na tukio hilo kabla ya kuwachukulia hatua kali," imeeleza taarifa hiyo.