Mchezaji Aziz K na Kocha Roberto Oliveira Watangazwa Kuwa Mwezi Octoba Ligi Kuu


Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, imemtangaza kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba, akiwapiga vikumbo Moses Phiri wa Simba, pamoja na Max Nzengeli wa Yanga, baada ya kupachika mabao manne kwenye dakika 278 za michezo minne aliyocheza kwenye mwezi huo.

Kwenye Taarifa hiyo, Bodi ya Ligi pia imemchagua Kocha wa Simba, Roberto Oliveira kuwa Kocha bora wa Mwezi Oktoba, baada ya kuingoza Msimbazi kushinda michezo dhidi ya Tanzania Prisons, Singida Fountain Gate, pamoja na Ihefu akiwaachia vumbi makocha Miguel Gamondi wa Yanga, pamoja na Abdulhamid Moalin wa KMC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad