Miamba Hawa Kutoka Simba Kuimaliza Yanga Kwa Mkapa, Kocha Robertinho Awakalisha Unyago

 

Miamba Hawa Kutoka Simba Kuimaliza Yanga Kwa Mkapa, Kocha Robertinho Awakalisha Unyago

 Miamba Hawa Kutoka Simba Kuimaliza Yanga Kwa Mkapa, Kocha Robertinho Awakalisha Unyago

Kocha Mkuu wa Simba Mbrazili, Robert Oliviera ‘Robertinho’ amewapa jukumu zito viungo wake wa kati Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin kuhakikisha viungo wa timu wa pinzani wasipate nafasi ya uumiliki mpira muda mrefu.


Hiyo ni katika kujiandaa na mchezo wa Kariakoo Dabi utakaopigwa Jumapili hii saa kumi na moja kamili kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar.


Safu ya kiungo ya Yanga hivi sasa inaundwa na nyota Khalid Aucho, Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli, Stephene Aziz Ki ambao ndio muhimili mkubwa wa timu hiyo.


Akizungumza nasi, Robertinho alisema maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa kuelekea Dabi hiyo, ambayo ni lazima waendele na rekodi nzuri ya kutopoteza.


Robertinho alisema amewaona wapinzani wake Yanga, ambao wapo bora katika safu ya kiungo, ambayo amepanga kuidhibiti kwa kuwapa jukumu viungo wake Ngoma na Kanoute aliyekuwepo katika kiwango bora hivi sasa.


Aliongeza kuwa anaamini ndani ya siku hizi tano kuanzia jana Jumatano hadi Jumamosi, viungo wake watashika maelekezo ya jinsi gani wanawazuia viungo wa Yanga, ili wakose muda wa umiliki mpira kwa muda mrefu.


“Maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa kuelekea mchezo wetu wa Dabi tutakaocheza dhidi ya Yanga, ni kati ya mchezo mkubwa kwangu ninakwenda kuucheza wenye historia.


“Yanga ni timu kubwa katika Ukanda wa Afrika, tunatakiwa kuingia kwa tahadhari kubwa kufanikisha ushindi katika mchezo huu, malengo yetu ni kupata ushindi siyo kitu kingine.


“Nimewaona Yanga katika baadhi ya michezo yao waliyoicheza ya ligi na kimataifa, pia nilikutana nao katika Ngao ya Jamii, hivyo tumejipanga vema kupata ushindi,” alisema Robertinho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad