Mke Ajitoa Uhai Kwa Kunywa Sumu Kisa Kuona Meseji ya Mapenzi Katika Simu ya Mumewe



Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa Jina la Marietha Bosco Sagana (32) mkazi wa kitongoji cha Matarawe, kijiji cha Marungu kata ya tingi tarafa ya mpepo wilaya ya nyasa Mkoani Ruvuma amefariki Dunia baada ya kunywa sumu chanzo kikiwa ni wivu wa Mapenzi.

Akizungumza na Wasafi Media Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma ACP-Marco Chilya, amesema tukio limetokea Novemba 8,2023 Majira ya Saa mbili za Usiku, siku ya tukio Mume wake alikuwa ameenda Shambani lakini alisahau simu yake Nyumbani Marietha alivyoiona simu hiyo iliyosahauliwa na mume wake akaanza kuipekua kwa kusoma Meseji zote ikiwemo za Whatsapp na akafanikiwa kukuta Meseji nyingi za Mume wake na Mwanamke Mwingine.

Marehemu baada ya kusoma Meseji hizo alishindwa kuvumilia hivyo akachukua Dawa ya kuulia Wadudu kwenye mahindi (Actellic ) akaikoroga na kuinywa na baadaye Marehemu aliishiwa nguvu majirani walipofika nyumbani kwakwe na walipomuuliza nini tatizo alisema amekunywa Dawa ya kuulia wadudu kwasababu ya meseji ambazo amezikuta kwenye simu ya mume wake ,wakati wanamkimbiza hospital njiani Marietha alifariki Dunia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad