Mwanaume Mtanzania Akiri Kufanya Sajari Kutoa Uume na Kujibandika uke

 

Mtanzania akiri kufanya sajari kutoa uume na kujibandika uke

Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Dayon ambaye ni Mtanzania na mkazi wa Arusha ingawa kwa sasa anaishi nchini Canada amewashangaza watu baada ya kubadili jinsia kutoka kwenye uanaume na kuwa mwanamke.


Tukio zima la kufanya mabadiliko hayo linapatikana kwenye Mange Kimambi App. Baada ya Watanzania wengi kulaani kitendo hicho, Dayon amewashukia na ujumbe huu.


"Aisee huku nilipo nikisema nimetokea Tanzania kitu cha kwanza watu wanasema ni nchi yenye upendo, siku zote nimekuwa nikijifurahia kusema natokea Tanzania. Ila kiukweli kabisa Watanzania mlioko huku Instagram sijui sio Watanzania ama sijui.


"Mimi nimeonyesha safari yangu ya kuwa mtu niliyetamani kuwa toka nikiwa na miaka 7, 8 hadi ukubwani nilitaka kuwa mwanamke siyo kwa sababu ya pesa, kwetu kila kitu tulikuwa navyo tayari.


"Mimi nimezaliwa Tanga mama akiwa mfanyakazi wa Serikali tena anayemfuata boss wa bandari ya Tanga, mama yangu amenifunza kupenda watu na kuwaheshimu hata kama ni wezi, nimetoka kwenye familia ya upendo maisha yalikuja kubadilika baadaye ila haikunibadilisha mimi.


"Maamuzi niliyofanya ya kufanya surgery ya kuondoa uume na kubandikwa uke ni maamuzi yangu binafsi siyo maamuzi ya taifa wala maamuzi yenu, na kama ikiwa mbaya ni mimi ndio nita suffer sio nyie, sasa why mnachukizwa na mtu ambaye hamumjui?


"Kuna wengine hadi wananiombea kifo eti Mungu aje aniue, mimi nipo karibu sana na Mungu, Mungu huyu alinitoa mahabusu ya Monduli na kuninyanyua na niko hapa na wale wote walio tekeleza ubaya nifungwe walikosa kazi zao na wengine kushushwa vyeo na uhamisho.


"So jueni Mungu anafanya kazi tofauti, alafu huyu Mungu kanitoa huko na kunileta huku na kanipa nafasi nyingine kimaisha, so watu jueni mimi huongea na Mungu kila siku kabla ya kufanya jambo lolote.


"Nilimuomba Mungu naomba upasuaji wangu usiwe na complications na ikawa hivyo hivyo, ninapona na ninapona tena alafu nyie mko bize mnampangia Mungu aniue, Mungu akawafunge midomo yenu na azidi kuwabariki, mimi siombei mtu ubaya hiyo ni kazi yake Mungu," ameandika Dayon.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad