Mwigizaji wa Nigeria MR Ibu Akatwa Mguu Kuokoa Maisha yake

'
Mwigizaji wa Nigeria MR Ibu Akatwa Mguu Kuokoa Maisha yake

'Kufikia saa saba mchana leo(jana), Baba yangu amefanyiwa upasuaji mara 7 hata hivyo ili kuokoa maisha yake na kuongeza uwezekano wake kupona, ilibidi mguu wake mmoja ukatwe.”


“Tukio hili limekuwa gumu kwetu sote lakini imetubidi tukubali ukweli huu mpya wa hali ya baba ili kumuweka hai.''

Mchekeshaji nguli raia wa Nigeria Mr IBU amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kufanyiwa upasuaji mara 7 na kukatwa mguu wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram familia ya mchekeshaji huyo ambaye jina lake halisi ni John Okafor imewomba Wanigeria wote wamuombee dua mbali na kumchangia fedha za matibabu.

Mr IBU alianza kuugua tangu mwezi Oktoba na ameonekana katika video moja akiwa amelazwa hospitalini, akiomba msaada wa kifedha.

Ugua pole Mr IBU, Je ni filamu gani unaikubali kutoka kwake?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad