Nyota Nane wa Yanga Waitwa Taifa Stars

Nyota Nane wa Yanga Waitwa Taifa Stars


Nyota wanane wa Kikosi cha Yanga Sc wamejumuishwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Niger na Morocco.

Kikosi hicho kilichoitwa na Kocha Mkuu, Adel Amrouche, kina jumla ya wachezaji 35.

Wachezaji hao waliojumuishwa kwenye kikosi hicho ni makipa wawili, Aboutwalib Mshery na Metacha Mnata.

Mabeki wapo wanne ambao ni Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Hamad na Nickson Kibabage.

Katika eneo la kiungo, yupo Mudathir Yahya, huku mshambuliaji akiitwa Clement Mzize.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad