Polisi: Hatujapokea Ripoti Baada ya Mwili wa Mohbad Kufukuliwa

Polisi: Hatujapokea Ripoti Baada ya Mwili wa Mohbad Kufukuliwa


Jeshi la Polisi la Jimbo la Lagos limetoa taarifa kwamba ripoti ya upasuaji ya marehemu mwimbaji, Ilerioluwa Aloba maarufu kama Mohbad, haijatolewa kwao.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alifariki mnamo Septemba 12 katika mazingira yenye utata. Wananchi wa Nigeria walitaka upasuaji ufanyike ili kujua sababu halisi ya kifo chake.

Septemba 21, hadi kufikia leo imetimia miezi miwili tangu mwili wake ufukuliwe ulipozikwa Ikorodu, jimbo la Lagos kwa ajili ya uchunguzi wa maiti. Ambapo Oktoba 6, amri ya polisi ilitangaza uchunguzi wa maiti ulikuwa umehitimishwa huku matokeo yakisubiriwa.

Msemaji wa Polisi, SP Benjamin Hundeyin, jana Jumatatu, Novemba 20, alisema bado haijapokea matokeo.

“Ripoti ya upasuaji haijatufikia. Baadhi ya watu wamekuwa wakisambaza uvumi kwamba tayari ipo. Ni jambo moja kuwa tayari, ni jambo lingine kuletwa kwetu rasmi, kwamba tutapokea na kusaini nakala tukithibitisha kuipokea. Kwa hiyo, hatufanyi kazi na uvumi, tunafanya kazi na ukweli”.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad