POLISI:Tunamshikilia Sheikh Ponda Kwa Mahojiano

POLISI:Tunamshikilia Sheikh Ponda Kwa Mahojiano

Jeshi la Polisi Kanda Maalum linamshikilia Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda kwa tuhuma za kupanga maandamano bila kufuata taratibu za Kisheria, ambapo maandamano yalipangwa kuanzia Viwanja vya Mnazi Mmoja hadi Manzese

Akizungumza na JamiiForums, Kamanda wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema “Awali, tulimueleza (Ponda) kuhusu utaratibu kuwa anatakiwa kutoa taarifa kwa Mkuu wa Polisi Wilaya, hakufanya hivyo, tukaona anahamasisha mitandaoni na baadaye kukusanya watu"

Ameongeza “Tunamhoji kinachoendelea na anatoa ushirikiano, kwani walitaka kuandamana kuhusu masuala ya vita inayoendelea Palestina, tukiruhusu hivyo na wengine pia watataka kuandamana kuhusu mataifa mengine. Baada ya mahojiano tutaangalia dhamana kwa mujibu wa Sheria.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad