Professor Jay: Wakati Niko ICU Nilishuhudia Vifo Vingi Sana

 

Professor Jay: Wakati Niko ICU Nilishuhudia Vifo Vingi Sana

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Professor Jay amedai kuwa kipindi alipokuwa mahututi ICU alishuhudia vifo vya wagonjwa wengi sana.


Akizungumza na chombo cha habari leo asubuhi msanii huyo ameeleza kuwa ingawa magonjwa ni ibada lakini watu wanakufa sana huko ICU tofauti na watu wanavyodhani.


Professor Jay anaeleza kuwa ndani ya siku 127 akiwa ICU ameshudia vifo vya watu wengi na amedai kuwa ukijikuta uko ICU una-survive hata kwa mwezi mmoja siyo mchezo.


Ikumbukwe kuwa taarifa za msanii huyo kuumwa zilianza kusambaa Januari mwaka 2022, na May 4 mwaka huu aliweza kuonekana tena akiwa mzima na kuendelea na majukumu yake kama awali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad