Rais Rais Samia Atoa Ndege Kuisafirisha Taifa Stars

Rais Rais Samia Atoa Ndege Kuisafirisha Taifa Stars


Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa ndege itakayotumika kuwasafirisha nyota wa timu ya Taifa (Taifa Stars ) kwenda Nchini Morocco ambako itaumana na Timu ya Taifa ya Niger katika kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ijayo ya Kombe la Dunia.


Taarifa ya Katibu mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Gerson Msigwa (@MsigwaGerson ) kwenye mitandao ya kijamii imesema: "Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan atoa ndege kwa ajili ya kuisafirisha Timu ya Taifa ya Soka kwenda Marrakesh Morocco ambako itaumana na Timu ya Taifa ya Niger katika kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ijayo ya Kombe la Dunia."


"Tunakushukuru sana Mheshimiwa Rais, sasa timu itasafiri kwa muda mfupi kwenda Marrakesh tarehe 16 Novemba, 2023 na itarejea haraka tarehe 19 Novemba, 2023 baada ya mchezo wake wa tarehe 18 Novemba, 2023 dhidi ya Niger.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad