Rais Samia Afanya Uteuzi wa Mabalozi

 

Rais Samia Afanya Uteuzi wa Mabalozi

 Rais Samia Afanya Uteuzi wa Mabalozi

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi James Gilawa Bwana kuwa Mwakilishi wa Tanzania nchini Afrika kusini.


Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imesema Balozi Bwana anachukua nafasi Balozi Meja Jenerali Gaudence Salim Milanzi ambaye amestaafu.


Lakimi pia amemteua Balozi Said Hussein Massoro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, akichukiua nafasi ya Balozi Said Shaib Mussa ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhra Yunus, aliyoitoa leo Novemba 9, 2023, huku akisema uteuzi huo unaanza mara moja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad