kufatia sakata la aliyekuwa Naibu waziri wa katiba na Sheria Paulina Gekuu kutuhumiwa kufanya shambulio la kikatili kwa vijana wawili ambao walikuwa wafanyakazi wake,
sakata hili ambalo limeshika vichwa vya habari katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari nchini Tanzania pamoja na matamko mbalimbali ya wanaharakati huku tukishudia jumuiya ya umoja wa wanawake ya ccm Uwt ikitoa tamko dhidi ya jambo hili .
Katika uchunguzi wake kuhusu Sakata hili TUmefanikiwa kupata jumbe (sms) kwenye Mfumo wa Screenshoot kati ya Mwenyekiti wa Chadema Babati Vijijini Paulina Narsis kwenda Kwa Mdogo wake Mbunge huyu Emannuel Gekuu akiombwa Pesa kiasi cha shilingi milioni tano ili kuzuia jambo kubwa linaloandaliwa dhidi ya mbunge huyu