Sabaya Ameshinda Hukumu Ya 3, Waliomshitaki Wameonekana Waongo Mbele Ya Majaji 3 Atoa Shukrani

Sabaya Ameshinda Hukumu Ya 3, Waliomshitaki Wameonekana Waongo Mbele Ya Majaji 3 Atoa Shukrani – Video

Mahakama ya Rufani imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na Upande wa Jamhuri na kueleza kwamba hakukuwepo na tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha, badala yake mjibu rufani wa kwanza, Lengai Ole Sabaya, alikuwa katika majukumu yake halali ya kufuatilia makosa ya uhujumu uchumi kama ilivyoelezwa na mashahidi wenyewe wa upande wa mashtaka.

Mahakama hiyo iliyokaa chini ya mwenyekiti wake, Jaji Jacob Mwambegele imeeleza zaidi kwamba mahakama ya hakimu mkazi iliyomtia hatiani Sabaya na wenzake ilikosea kutochambua ushahidi unaoonyesha wazi kwamba, haijawahi kutokea jambazi amkamate mtuhumiwa, amnunulie ndizi na baadae kumpeleka polisi kama mashahidi wenyewe walivyoelezea kutendewa na Sabaya.

Hukumu hiyo ilimaliza kwa kusema haipingi maamuzi ya mahakama kuu yaliyomuweka huru Sabaya na wenzake hao na kufutiwa kifungo cha miaka 30.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad