Salim Kikeke Afunguka Kuacha Kazi Kisa Kuja Kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali

Salim Kikeke Afunguka Kuacha Kazi Kisa Kuja Kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali


Mtangazaji na Mwandishi nguli wa habari aliyefanya kazi katika Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC) kwa miaka 20, Salim Kikeke @salim_kikeke amesema hakuwa na makubaliano na Serikali ya Tanzania kwamba aache kazi na arudi Tanzania kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali bali alirejea baada ya kuona ni wakati sahihi kwake kurudi nyumbani.


“Habari hizo zingekuwa na ukweli sasa hivi ningekuwa Mfanyakazi wa Serikali lakini nashukuru kama Watu wanaweza kunipa nyadhifa kama hizo, sikuwa na makubaliano yoyote na Serikali wakati naacha kazi na sina makubaliano yoyote na Serikali kama itatokea basi itatokea baadaye lakini nilirudi kwa uamuzi wangu mwenyewe na nilisema nitarudi”


Salim amesema hayo kwenye mahojiano maalum na Mwandishi wa @AyoTV_, Ramadhani Mwelondo ambapo amesema amerejea Tanzania kwa ridhaa yake baada ya kuomba zaidi ya mara moja kuacha kazi kwa hiyari yake lakini je ni ipi sababu hasa ya kurejea nchini? anatamani kuingia kwenye siasa? yote amefunguka na tayari full interview ipo Youtube ya millardayo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad