Serikali Yakiri Walioshauri Ujenzi wa Daraja la Jangwani na Miundo Mbinu Waliikosea

 

Serikali Yakiri Walioshauri Ujenzi wa Daraja la Jangwani na Miundo Mbinu Waliikosea

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamedi Mchengerwa amekiri kwamba walioshauri ujenzi wa mradi eneo la Jangwani ikiwemo daraja na miundombinu mingine kwa namna ilivyo sasa waliikosea Serikali lakini amesema wanakiri makosa huku wakijisahihisha na kwamba sasa Serikali ya awamu ya sita tayari imesaini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza mapema iwezekanavyo.


“Lazima tukiri kwamba waliotushauri tuijenge Jangwani kwa namna ilivyo sasa walitukosea lakini tukiri makosa huku tukijisahihisha,

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu tayari imesaini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza mapema iwezekanavyo”


Amesema hayo wakati wa ziara ya pamoja aliwa na Mawaziri wa Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Fedha ambapo wametembelea eneo la Jangwani ambalo limeathirika na mvua zinazoendelea kunyesha baada ya Mto Msimbazi kujaa ambapo amesema mradi wa uboreshaji wa Mto Msimbazi unaotegemewa kuanza hivi karibuni utatatua changamoto za miaka 100 ijayo na sio baada ya miaka 10 tena kuwe na changamoto kama za sasa .


Amesema tayari Serikali kupitia OR-TAMISEMI imesaini mkataba wa kupata fedha kutoka Benki ya Dunia zitakazo wezesha kutekeleza mradi mkubwa wa uboreshaji wa Bonde la Mto Msimbazi ikiwa ni pamoja na kujenga daraja la juu litakaloanzia eneo la Magomeni hadi njia panda ya Muhimbili (Fire) ambao umepangwa kuanza Februari 2024.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad