Ili kuepuka au kupunguza Madhara ya Kiafya yanayoweza kuletwa na mvua kubwa au mafuriko, Wizara ya Afya imetoa wito kwa Wananchi kukaa mbali na mitaro ya maji, nguzo za umeme, kuta za nyumba na maeneo mengine hatarishi
Pia, Kutoruhusu Watoto kucheza ndani au karibu na maji ya mafuriko, kutojaribu kuogelea, kutembea au kuendesha gari kwenye maji. Wananchi wanatakiwa kuweka vizuia maji mfano mifuko ya mchanga katika kuta za nje ya nyumba na maeneo ya wazi ya ikiwemo kwenye milango lakini wasipange mifuko ya mchanga kwa kuegemeza katika kuta za nyumba
Kutokana na mvua zinazoendelea, Mdau hali ya Mazingira ipoje Mtaani kwako?