Serikali Yawatoa Hofu Wananchi, Taarifa Mgonjwa Mpya wa Surua

Serikali Yawatoa Hofu Wananchi, Taarifa Mgonjwa Mpya wa Surua


Halmashauri ya jiji la Dodoma imesema hakuna mgonjwa mwingine aliyethibitika kuugua ugonjwa wa Surua, baada ya uwepo wa taarifa za watu wanne wa awali, wanaotoka katika familia moja kupatiwa matibabu.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Best Magoma, amesema jamii haina haja ya kuogopa kwa sababu Serikali imedhibiti hali na ameongeza kuwa.“ Hakuna haja ya jamii kuwa na hofu wala taharuki kwani kwa hali ilivyo sasa bado tunaweza kufanya udhibiti na kwamba tunaendelea na ufuatiliaji wa kutoa elimu kwa jamii.”

Amesema,wanaendelea kufanya ufuatiliaji katika jamii kubaini ikiwa kuna yeyote mwenye dalili kama hizo. Miongoni mwa miito inayoendelea kutolewa hivi sasa ni wazazi kuchanja watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

“Vituo vyetu vyote vipo tayari kuendelea kutoa huduma za chanjo bila gharama zozote, na tunahitaji kuchanja idadi kubwa zaidi ili kupunguza uwezekano wa kutokea kwa mlipuko baadaye” Alisema.


Ugonjwa wa surua, husababishwa na virusi aina ya “Morbillivurus paramyxvirus” vinavyoenea kwa haraka kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine,na huenezwa kwa njia ya hewa pale mgonjwa anapokohoa au kupiga chafya.


Ugonjwa huuhuathiri watu wa rika zote,licha watoto wenye umri chini ya miaka mitano ndio huathirika zaidi. Saa 24 zilizopita halmashauri ya jiji la Dodoma lilitoa tahadhari ya kuwepo kwa mlipuko wa surua na kutoa wito wa jamii kuchanja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad