Shaffih Dauda 'Zingatia Vitu Hivi ili Ufanye Vizuri Uwanjani'

Shaffih Dauda 'Zingatia Vitu Hivi ili Ufanye Vizuri Uwanjani'


 Sehemu kubwa ya wachezaji tunaowaona huko duniani ,wamezaliwa na vipaji lakini hawakutosheka na vipaji pekee , unaweza kuwa mchezaji lakini usifikie daraja la kuwa mchezaji bora kama hakuna juhudi binafsi za kujiongezea maarifa , ubora na Ukamilifu wa mchezaji wa mpira unajengwa na vitu vikubwa vinne ! ukiwa kama mchezaji na una ndoto ya kuwa mchezaji hauwezi kuvikwepa !


1. Consistent training

Muendelezo kwenye mazoezi , hauwezi kuwa bora kama utakuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi kwa kujitegea ! Wapo wachezaji wana uwezo wa kuzaliwa nao lakini ukamilifu wa mchezaji kamili ni lazima awe fit , ufit haupatikani nje ya mazoezi ni sawa na kusema practice doesn’t make perfect ,perfect practice dose .


2. Mental toughness .

Mchezo wa mpira wa miguu unabebwa sana na utimamu wa akili , kadri unavyoiweka akili mchezoni ndivyo inavyokupa uhakika wa game bora! mara kadhaa utasikia mchezaji fulani hatokuwa sehemu ya mchezo kwa sababu ya matatizo ya kifamilia ,vipo vitu wanaangalia kama utakuwa uwanjani na akili yako ipo nyumbani ni ngumu kutoa kilichokusudiwa , kama mchezaji unatakiwa kuwa bora pia eneo hili


3.Physical fitness

Maarifa na mbinu vina nafasi kubwa sana uwanjani lakini urahisi wa kuhamisha kilicho kwenye mawazo kuwa uhalisia uwanjani inakuhitaji kuwa na utimamu wa mwili , sehemu inayohitaji ukakamavu kulinda mpira fanya hivyo , inapohitajiks kasi kimbia ! So kama mchezaji unatakiwa kuwa na ratiba bora ya mazoezi ya utimamu wa mwili ili kumudu kila tukio kwa ukamilifu.


4.Study the game

Hii ni sehemu ya mbinu , zipo mbinu utapewa na mwalimu lakini zipo mbinu zitakuhitaji wewe mwenyewe kujiongeza. Kama mchezaji tenga muda wa kujiongezea mbinu na maarifa , njia za kujiongezea mbinu zinaweza kuwa kuangalia mechi tofauti tofauti, kuangalia wachezaji wakubwa wa nafasi yako wanatafsiri vipi matukio ,mwisho yafanyie kazi maarifa unayoyapata nje kuongeza kitu kwenye career yako !


Hivi ni vitu vinne muhimu ambavyo watu wa mpira wanapaswa kufahamu hasa wachezaji ili kujijenga na kuwa bora kila wakati .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad