Simba SC yataja sababu kuchelewa kupata kocha




Uongozi wa Simba SC umevunja ukimya kwa kueleza kilichokwamisha katika mchakato huo wa kumpata Kocha Mkuu Mpya wa kikosi chao katika kipindi hiki cha kuelekea mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza wa Kundi B, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast,

Simba SC walijinasibu kumtangaza Kocha Mkuu mpya atayerithi nafasi ya Robertinho kabla ya mchezo huo, na kuwajaza matumaini Mashabiki na Wanachama wao, lakini imekuwa tofauti, huku siku tatu zikisalia kuelekea mchezo huo wa Kimataifa.

Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally, amesema mchakato huo umechelewa kutokana na umakini mkubwa ambao unachukuliwa na Uongozi wa juu wa klabu hiyo, ili kumpata Kocha Mkuu mwenye sifa stahiki za kuipeleka mbali timu yao.

Amesema hawataki kufanya jambo hilo kwa haraka kwa sababu wanahitaji kufanya maboresho makubwa kwa kuleta mtu ambaye wataenda naye sawa kwenye mipango yao ya muda mrefu.


Amesema wanahitaji kuwa watulivu katika mchakato huo wa kupata mtu aliyekuwa sahihi ambaye atakuja kwa ajili ya kwenda nao katika njia moja, hivyo wanahakikisha wanapata kocha bora mwenye vigezo walivyojiweka.

“Tumeona kuna makocha wengi wakitajwa akiwamo Benchikha ni kocha mzuri, hakuna sehemu viongozi wa Simba SC wamemtaja, mchakato umechelewa kwa sababu ya kutohitaji kupata kocha baada ya mechi mbili tunamwondoa.

“Kuepukana na hilo tumelazimika kuwa makini katika mchakato huu. Tunawaomba mashabiki na wanchama wetu kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho wana shauku ya kumfahamu Kocha Mkuu mpya wa kikosi chetu.


Makocha wengi wanahusishwa kuja kuchukua nafasi ya Robertinho akiwamo Sven Vandenbroeck, Abdelhak Benchikha, ambaye alikuwa chaguo la kwanza, lakini imeshindikana kutokana na dau kubwa analohitaji na mwingine Fernando Da Cruz pamoja na Radhi Jaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad