Simba waingia mtego wa ASEC Mimosas, walazimishwa sare kwa Mkapa

 

Simba waingia mtego wa ASEC Mimosas, walazimishwa sare kwa Mkapa

Simba imeanza kwa kasi ndogo mechi ya kwanza hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.


Simba ilitumia vyema dakika 45 za kwanza kupata bao la kuongoza mfungaji akiwa Said Ntibazonkiza 'Saido' dakika ya 44 kwa mkwaju wa penalti.


Penalti hiyo imetokana na beki wa ASEC kuunawa mpira wakati akitaka kuokoa shuti la mshambuliaji Kibu Denis.


Bao hilo lilidumu kwa kipindi hicho na kuifanya Simba kutoka wakiwa na uongozi wa bao 1-0 huku pia wakiwadhibiti vizuri wapinzani wao.


Hata hivyo Simba ingeweza kupata mabao ya kutosha lakini wachezaji wake wakashindwa kutulia kumalizia nafasi ambazo wametengeneza kupitia Kibu, Mzamiru Yassin na Jean Baleke.


Kipindi cha pili Simba ilirudi na kasi katika dakika 10 za kwanza kujaribu kutafuta bao la kuutanua uongozi wao lakini ASEC Ikawa makini kuwadhibiti


ASEC ikaamka na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 77 mfungaji akiwa Serge Pokou akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji William Sankara.


Simba baada ya bao hilo wakaonekana kushindwa kuiongezea presha ASEC kupata bao la ushindi.


Licha ya Simba kufanya mabadiliko matano kwa kuwaingiza Clatous Chama, Mosses Phiri, Sadio Kanoute, John Bocco na Luis Miquissone wakichukua nafasi ya Jean Baleke, Kibu Denis, Che Malone na Saido bado hawakuweza kupata bao.


Mpaka mwisho wa mchezo Simba ikajikuta inalazimishwa sare dhidi ya ASEC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad