Simba Wanamtaka Kocha wa Klabu ya USM Alger, Waanza Mazungumzo

 

Simba Wanamtaka Kocha wa Klabu ya USM Alger, Waanza Mazungumzo

Klabu ya Simba imefanya mazungumzo rasmi na aliyekuwa Kocha wa Klabu ya USM Alger, Abdelhak Benchikha ili kuona iwapo kutakuwa na uwezekano wa kipata huduma yake.


Simba sasa inasaka kocha mpya kabla ya kuanza kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi kufuatia kumtimua aliyekuwa kocha wao, Roberto Oliveira 'Robertinho' raia wa Brazil baada ya kipigo cha bao 5-1 kutoka kwa Yanga.


Benchikha ambaye ni raia wa Algeria ndiye alikuwa mwiba kwa Profesa Nasreddine Nabi na zyanga msimu uliopita baada ya kufanikiwa kushinda na kunyakua kombe la Shirikisho Afrika wakati wa fainali baina ya timu hizo, baada ya kulingana idadi ya mabao na mshindi akaamriwa kwa kanuni.


• CAF Confederation Cup

• CAF Super Cup


Makocha wengine wanaotajwa ni Sven Vandenbroeck na Didier Gomes Derosa ambao waliwahi kuifundisha Simba SC kwa mafanikio hapo nyuma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad