Simba Watulie Sasa, Wampe Muda Kocha Benchikha

Simba Watulie Sasa, Wampe Muda Kocha Benchikha

Simba Watulie Sasa, Wampe Muda Kocha Benchikha

Juzi usiku mabosi wa Simba walimtangaza rasmi kocha wao mpya Abdelhak Benchikha ambaye alikuwa na msaidizi wake Farid Zemiti na kocha wa viungo Kamal Boudjenane.


Hao wamekuja baada ya watangulizi wao kuvunjiwa mikataba yao kutokana na matokeo waliyoyapata kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, Simba ikifungwa mabao 5-1.


Hata hivyo, mabosi wa Simba walikuwa hawafurahishwi na mwenendo mzima wa timu yao chini ya benchi lao la zamani hivyo kufikia makubaliano ya kuvunja mikataba hiyo.


Makocha hao wamekuja ikiwa zimebaki siku chache Simba kwenda kucheza mechi ya pili ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwanang ya Botswana itakayochezwa Desemba 2, mwaka huu.


Mashabiki wa Simba wamepoteza imani na kikosi chao, hawaamini katika ubora wao wanaweza kuwapata matokeo mazuri siku zijazo kutokana na ugumu wa mashindano hayo ikiwemo ushindani wa ligi ya nyumbani.


Mashabiki wa Simba wanaona wachezaji wao viwango vyao vimeshuka ama vinaendelea kushuka kadri siku zinavyosonga mbele huku yakiwepo mambo mengi yaliyojitokeza siku za hivi karibuni ambayo yamewakatisha tamaa.


Ukiwaangalia mashabiki wa Simba hata pale timu yao inapata matokeo mazuri lakini hawana furaha madai yao hawaoni ule ubora wa kikosi chao hivyo ni kama vile matokeo mazuri wakipata wanakuwa kama wamebahatisha.


Sasa amekuja kocha mpya, kocha ambaye wanaamini ni wa viwango vya juu ambaye anaendana na ukubwa wa Simba, kaja na kikosi chake na ataamini kwenye falsafa zake kutengeneza timu.


Benchikha ni kocha mwenye CV kubwa anaonekana kafundisha timu kubwa zenye mafanikio makubwa Afrika na analifahamu vyema soka la Afrika lakini amekuja kipindi kibaya ambacho tayari timu ya Simba imevurugika haina muunganiko unaelekewa.


Kocha huyo amefika kipindi ambacho hata wakifanya usajili basi ni kwa asilimia ndogo maana ni dirisha dogo lililopo mbele yake hawezi kufumua kikosi kizima ama hawezi kupata wachezaji bora kwa sasa maana wengi wapo kwenye mikataba na timu zao.


Amekuja kipindi ambacho atahitaji utulivu na kuwatumia zaidi wachezaji waliopo na sio wale anaowahitaji yeye kwa wakati huo, waliopo ni kuhakikisha kwenda nao katika mbinu zitakazompa matokeo mazuri.


Wakati yote hayo anakumbana nayo Benchikha basi viongozi na mashabiki wa Simba wanahitaji kuwa na utulivu wa hali ya juu na kuvumilia kila hali, maana hata mashabiki wakipiga kelele za kumfukuza kama hawaoni matokeo mazuri hazitasaidia kutokana na nyakati zilizopo.


Benchikha na benchi lake wana kazi ya ziada ya kufanya ndani ya Simba ili kukitengeneza kikosi chake maana ukiachana na kiwango chao lakini inaonekana ndani ya timu hakuna ule umoja, hivyo ni kazi ya ziada kuurejesha umoja na kila mmoja kujiona ni sehemu ya timu.


Simba inahitaji mafanikio makubwa zaidi lakini kwa kinachoendelea sasa wanapaswa kuanza kusaka mafanikio makubwa msimu ujao ili msimu huu wampe nafasi kocha wa kujenga na kutatua yaliyopo kwa wachezaji wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad