Wakati Bodi ya Bonde la Wami Ruvu ikitoa tahadhari ya mafuriko kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, tayari athari zimeanza kujitokeza.
Tahadhari hiyo ilitolewa kwa maeneo ya Gongo la Mboto, Ulongoni, Vingunguti, Tabata Matumbi, Darajani, Jangwani na Miyombo-Kilosa mkoani Morogoro.
Katika taarifa ya bodi hiyo iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, inawajulisha wakazi wa maeneo hayo kuwa kuna uwezekano wa kupata mafuriko kati ya Novemba 2 hadi 9, mwaka huu.