Andiko la @dericklissu
Ukweli ni ufunguo ! utakuweka wazi na kukurekebisha makosa lakini pia utakusaidia kujua njia sahihi ya kupita.
Kibaya ni kwamba mashabiki,watawala na washika dau wanapenda uwasifie hata kama hawapo vizuri,hawataki kusikia madhaifu yao utajiuliza tutafika kweli kwa namna hili?
Scouting,menejimenti na benchi la ufundi ni kweli mnakaa pamoja na kujadili nani atatufaa kwa wakati huu na kufiti nafasi ya aliyetoka kwenye plan za kocha na falsafa ya soka letu ?
Binafsi sikuona haja ya kumrejesha Luis Miqussione,sahihi alifanya vizuri wakati ule lakini ninachojua uwezo unapungua na kuongezeka kadri unavyotumika na usivyotumika
Kila siku vipaji vipya hujitokeza na kufanya vizuri,
kwamba hawakuona wachezaji wengine sokoni mpaka wakamrejea yeye? au pengine kwakuwa ilikuwa rahisi kumpata?
Simba ni klabu yenye kumsajili mchezaji ili kuisaidia timu moja kwa moja,sio akasubiliwa mpaka awe vizuri,mchezaji kuja kuanza kikosi cha kwanza na kuchagiza ushindi .
Mpaka sasa Miqussione kwenye michezo 6 ya Ligi Kuu NBC Premier League ameanza mmoja tu dhidi ya Coastal Union,dhidi ya Mtibwa Sugar alikuwa benchi,dhidi ya Dodoma Jiji, dhidi ya Tanzania Prison hakuwepo hata benchi,dhidi ya Singida Fountain Gate alikuwa benchi,dhidi ya Ihefu hakuwepo ata benchi.
African Football League mchezo dhidi ya Al Ahaly wa kwanza alianza mchezo wa pili hakuwepo hata kwenye kikosi cha wachezaji wa akiba lakini pia CAF Champions League dhidi ya Power Dynamos FC hakuwepo hata benchi
Kwahiyo karibu michezo mingi Luis Miqussione amekuwa na ingia toka nyingi,kitu ambacho sio kizuri kwa klabu na yeye mwenyewe.
Matarajio yalikuwa makubwa mnoo kwa mashabiki wake.