Tuhuma: Walimu wadaiwa kula Chakula cha Wanafunzi



Mkuu wa wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf amepiga marufuku vitendo vya Walimu kula chakula kinachopelekwa shuleni kwa ajili ya Wanafunzi, hali ambayo amesema inafifisha juhudi za wazazi katika kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao.


DC Jamila ametoa maagizo hayo 2023 katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC), kilichofanyika mjini Mpanda ambapo ameelezea kusikitikishwa kwake na na hali hiyo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wazazi na walezi.


“Natumia nafasi hii kupiga marufuku, kama kuna shule wana huo utaratibu kutum ia chakula kilichopelekwa kwa ajili ya wanafunzi ni marufuku kuanzia leo, nikipokea tena malalamiko nawakurugenzi mpo kwamba walimu kwanini na wao wasichangishane?” alihoji DC Jamila.


Hata hivyo, amewataka maafisa Tarafa kusimamia zoezi la utoaji wa chakula shuleni linakuwa la lazima na sio hiyari katika shule zote, ili kuhakikisha kama wanafunzi wanapata chakula shuleni bila kikwazo chochote.


Katika Hatua nyingine amewaagiza maafisa Watendaji wa Mitaa na Vijiji Wilayani humo, kuhakikisha wanasimamia zoezi la uandikishaji wa Wanafunzi wa darasa la kwanza na awali, pamoja na kusimamia wanafunzi wanaoripoti kidato cha kwanza mwaka 2024.


Amesema, watendaji wanao wajibu wa kuhamasisha wazazi na walezi kuhakikisha wanawaandikisha watoto wao shuleni na mtendaji ambaye eneo lake litakuwa chini ya asilimia 100 mwisho wa zoezi atachukuliwa hatua.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad