Ubabe wa Yanga Upo Kwenye Utatu Huu Mtakatifu...

 

Ubabe wa Yanga Upo Kwenye Utatu Huu Mtakatifu...

Yanga pale wana utatu wao kwenye safu ya kiungo unaitwa MAP ukimaanisha majina ya wachezaji Maxi, Aziz na Pacome.

Ni Maxi Nzengeli, Aziz Ki Stephane na Pacome Zouzoa ambao wanacheza pale katika mstari wa viungo watatu wa kushambulia wa Yanga na wamekuwa wakiutendea haki sana kwa ama kufunga mabao au kupiga pasi za mwisho.

Wakati wanakwenda kucheza mechi ya watani wa jadi, Simba walitahadharishwa na vyombo vya habari juu ya utatu huo na wakawekewa takwimu zao jinsi walivyo moto wa kuotea mbali hasa katika kipindi cha pili hususan zile dakika 30 za mwisho.

Kabla ya kucheza na Simba, utatu wa MAP ulikuwa umefunga mabao 14 kwenye ligi ambapo Aziz Ki alikuwa amepachika mabao sita, Nzengeli Maxi alikuwa amefunga mabao matano na Pacome yeye alikuwa amefumania nyavu mara tatu.

Katika kile kilichoonekana Simba hawakuchukua tahadhari dhidi ya hao jamaa watatu, wote walifunga mabao dhidi yao katika kichapo cha mabao 5-1 ambacho Yanga walikitoa kwa mtani wao Jumapili iliyopita pale Benjamin Mkapa.

Kwa hali inavyoonekana timu nyingi sana zitakumbana na maafa ya MAP kama zikiendelea na kuuchukulia poa utatu huo pindi zinapokutana na Yanga ama katika Ligi Kuu au mashindano mengine ya ndani au kimataifa.

Silaha ya kwanza kubwa ya timu kukabiliana na hao jamaa watatu ni kuwa na nidhamu kubwa ya mbinu pamoja na ufiti wa hali ya juu ambao utawafanya wachezaji wa timu pinzani kuweza kumudu presha ya kukabiliana na MAP katika dakika zote za mchezo.

Unapokutana na Yanga jambo la muhimu zaidi ni kuwapa heshima na kutotaka kupishana nao katika muda mwingi wa mchezo hasa unapokuwa na kundi kubwa la wachezaji ambao hawawezi kuendana na presha na nishati yao.

Kushindwa kuyafanya hayo ni kujitengenezea hatari kubwa dhidi ya Yanga na hapo ndipo timu itakapotengeneza mazingira ya kukutana na kibano cha MAP.

Katika mabao 28 ya Yanga hadi sasa msimu huu, MAP wamefunga mabao 18, ikiwa na maaba Aziz Ki, Max, wamefunga saba kila mmoja, huku Pacome akifunga mabao manne, na wote wanatokea kwenye eneo la kiungo ikiwa ndiyo timu yenye kombinesheni kali zaidi kweli Ligi Kuu Bara hadi sasa.

Hii ina maana, ukiwatoa hao watatu wenye mabao 18, mabao 10 tu ndiyo yamefungwa na wachezaji kutoka maeneo mengine kwenye timu hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad