Uhuru Kenyatta: Serikali ya RUTO Iache Kulaumu Serikali iliyopita, Wafanye Kazi

Uhuru Kenyatta, ruto

Rais Mstaafu wa Kenya, #UhuruKenyatta ameiambia Serikali iliyoko Madarakani iache kuulaumu Utawala wake kwa kushindwa kutimiza malengo iliyowaahidi Wananchi

Uhuru amesema “Kila mara Mtu anaposhindwa kufanya anachopaswa kufanya, analaumu Serikali iliyopita. Huu mwenendo hata kama Mke amekataa kujifungua, tutalaumiwa sisi, lakini tumezoea hili,”

Mapema Mwezi huu, Waziri wa Fedha, Profesa Njuguna Ndung’u aliilaumu Serikali iliyopita kwa chanzo cha gharama kubwa za Maisha. Wiki iliyopita, Waziri wa Uchukuzi, Kipchumba Murkomen naye aliilaumu Serikali iliyopita kwa Ujenzi wa Paa linalovuja katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa #JomoKenyatta


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad