Ummy Mwalimu 'Wanachi Wanauza Mali zao Kugharamia Matibabu"
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na Bima ya Afya ili kuwa na uhakika wa matibabu kabla ya kuugua.
Amesema baada ya Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote kupitishwa na kuwa sheria itasaidia Wananchi kupata matibabu hasa kwa wasio na uwezo.
Pia amesema Serikali itaendelea kutoa elimu na hamasa kwa Wananchi kuhusu dhana na umuhimu wa bima ya afya, lengo likiwa ni kuwaepusha Wananchi kuingia katika umaskini huku akitolea mfano baadhi ya Wananchi ambao walilazimika kuuza mali zao ikiwemo mashamba, mifugo, vyombo vya usafiri, vifaa vya ndani na kuweka rehani mali zao ili kugharamia matibabu yao au ya wapendwa wao.
Aidha, amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya katika ngazi zote ili kuwezesha Wananchi kupata huduma bora za afya.