Klabu ya Zamalek itatuma maafisa wake nchini Algeria katika mchezo wa CR Belouizdad dhidi ya Yanga kwa ajili ya kuwafuatilia kwa karibu Pacome Zouzoua raiabwa Ivory Coast na Maxi Nzengeli raia wa CongoDR.
Taarifa kutoka gazeti la Championi zinaeleza kuwa Maafisa hao inaarifiwa kuwa watatua pia Tanzania kuendelea kuwafuatilia wachezaji hao watakapokuwa wanacheza michezo ya kimataifa pekee katika michezo ya nyumbani ya Yanga.
Yanga watawafuata CR Belouizdad wiki ijayo kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa nchini Algeria, Ijumaa ijayo Novemba 24, 2023.
Maxi na Pacome wamekuwa viungo mwiba kwa mabeki wa ligi kuu kwani tangu wasajiliwe msimu huu na Yanga wameonyesha uwezo mkubwa jambo linalowafanya kuwa miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa na kocha Miguel Gamondi.