Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, timu ya Simba SC, imebanwa mbavu nyumbani kwa kulazimishwa sare ya 1-1 na Asec Mimosa ya Ivory Coast.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage amesema wachezaji wa timu hiyo wanaonekana kama wamechoka, hivyo ni lazima usajiri upya ufanyike dirisha dogo ili kuinusuru timu hiyo.
“Simba hawakucheza vizuri hata kidogo wanaonekana wamechoka sana hawana nguvu labda sijui wanawaza michezo ya nyuma, lakini Simba Sc wanahitaji kufanya usajili dirisha dogo, vinginevyo mambo ni magumu.
“Nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hii bado ipo lakini lazima Simba waingie sokoni dirisha dogo tena wafanye usajili mkubwa, la sivyo hatutatoboa,” amesema Rage.
Msimamo
Galaxy – goli 1, pointi 3, nafasi ya 1
Asec Mimosas – goli 1, pointi 1, nafasi ya 2
Simba Sc – goli 1, pointi 1, nafasi ya 3
Wydad goli 0, pointi 0, nafasi ya 4.
Mechi zijazo
Galaxy vs Simba
Asec vs Wydad
Tangu msimu huu umeanza, Simba haijashinda mchezo wowote wa Kimataifa.
Power Dynamo 2-2 Simba SC
Simba SC 1-1 Power Dynamo
Simba SC 2-2 Al Ahly
Al Ahly 1-1 Simba SC
Simba SC 1-1 Asec Mimosac.