Serikali imesema Wananchi 2,400 wanaopisha uendelezaji Bonde la Msimbazi tayari wameanza kulipwa fidia zao leo, hatua hii inakuja baada ya jana Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa kuongea na Wananchi wanaoathiriwa na uendelezaji wa Bonde hilo kwenye eneo la Jangwani jijini Dar es salaaam na kuwapa ahadi kuwa leo wataanza kulipwa.
Amesema fidia hiyo inalipwa kwa Wananchi wote waliokubali kulipwa na kufanyiwa uhakiki wa taarifa zao za kibenki ili kupisha utekelezaji wa mradi huo na tayari Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameshatoa fedha kwa ajili hiyo “Natambua kabisa wapo Wananchi asilimia 92 kati ya wote wanatakiwa kulipwa fidia wanasubiria fedha zao na sikatai wapo wengine wenye malalamiko Wataalamu wangu endeleeni kuyafanyia kazi na mkishindwa yaje kwangu nione hatua ya kuchukua”
Wananchi wa Mitaa 16 wameanza kulipwa malipo mbalimbali kutokana na thamani ya vitu walivyonavyo ambapo malipo hayo yanajumisha kifuta jasho, usumbufu, mali pamoja na kodi ya nyumba ya miaka mitatu kwa wale waliokuwa na nyumba eneo hilo na wanaishi ili wapate fedha za kulipia kodi ya nyumba kipindi wanaendelea na ujenzi,.