Watu Mnaoitetea Bangi Tanzania Tutawasaka Mpimwe

Watu Mnaoitetea Bangi Tanzania Tutawasaka Mpimwe


Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo amewataka Watanzania wote kujiepusha kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi kwa kutumia mavazi, maneno na hata mitandaoni wakiwemo wale ambao comment zao mitandaoni na mitaani huonesha kutetea dawa hizo ambapo amesema atakayefanya hivyo atapimwa na akibainika anatumia dawa hatua zitachukuliwa.


Akiongea Jijini Dar es salaam, Lyimo amesema “Maabara yetu ya kisasa ikikamilika tu tutashughulika na wote yaani Mtu akihamasisha tu matumizi ya dawa za kulevya tunamkamata tunaenda kumpima tukikuta anatumia dawa za kulevya tunampeleka Mahakamani”


“Nitoe wito kwa Wananchi wote ambao kwa nafasi yoyote waliyonayo wanatumia kuhamasisha dawa za kulevya tuwaombe waache, kuanzia sasa hivi wale wote watakaokuwa wanahamasisha ikiwemo kwa mavazi, maneno na kwa kutumia majukwaa yao tutachukua hatua ikiwemo kuwapima ili kuhakikisha kama na wao wanatumia na tukikuta wanatumia sheria itachukua mkondo wake, maana huwezi tu kutetea kitu ambacho hautumii”


“Baada ya kutoa taarifa kwamba ukivuta bangi ubongo ukiharibika unawaza kuwaza visivyoonekana, nimeona Kituo kimoja cha Habari wanaanza kujadili na kusema kama tunaona visivyojulikana mbona Mimi ninatumia sijaviona hivyo vitu!?, sasa huyo Mwandishi wa Habari tutamtafuta ili tumpime kama kweli anatumia dawa za kulevya tuweze kumchukulia hatua kwasababu amejitangaza mwenye kuwa anatumia huo ni uhamasishaji wa matumizi ya dawa za kulevya”


“Huwa tunaenda Mikoani kuteketeza bangi, juzi kuna Kuna Mtu (Mbunge) akasema Bungeni kwamba sisi kazi yetu ni kupiga picha tu na selfie tukiwa tunateketeza bangi, ni kwakuwa tu Mbunge huyu kasemea haya Bungeni na wana kinga angesema nje ya Bunge tungempima na yeye ili kujiridisha kama na yeye ni Mtumiaji au laah”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad