Ahmed Ally:Clatous Chama Hataondoka Simba kikawaida Kama Mnavyodhani

 

Clatous Chama

Semaji la CAF, Ahmed Ally, amesema Clatous Chama bado ni mchezaji halali wa Simba SC na kama akiondoka basi atapewa heshima yake.


Amesema kwa sasa kesi yake ipo kwenye kamati ya nidhamu hivyo Wanasimba waipe muda kamati hiyo.


"Kesi ya Chama ipo kamati ya nidhamu ya Simba SC, lakini kwa kipindi hiki chote Chama anaendelea kulipwa stahiki zake kama kawaida kwa sababu ni mchezaji halali wa Simba.


“Chama ni mchezaji wetu na hatoondoka hivi karibuni, Chama ana mchango mkubwa wa Robo Fainali nne za Simba Klabu Bingwa Afrika hivyo hata ikififika wakati wa kuondoka Simba basi mjue hatoondoka kikawaida lazima tumpe heshima yake,” alisema Ahmed

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad