Aliyekataa Ndoa na Binamu yake Auawa

 
Aliyekataa Ndoa na Binamu yake Auawa

Aliyekataa Ndoa na Binamu yake Auawa

Wazazi wawili wenye asili ya Kipalestina (Shabbar Abbas na Naziah Shaheen) wamehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua binti yao Saman Abbas (18) aliyekataa kwenda Pakistan kwa ajili ya kuolewa na binamu yake.


Ripoti kwenye mitandao ya kijamii zinaeleza kuwa wazazi hao walikasirishwa na picha za binti yao akibusiana na mpenzi wake barabarani ili hali wao walitaka aolewe na binamu yake huko Pakistan.


Mwezi wa Novemba mwaka jana, mwili wa Saman Abbas uligunduliwa katika shamba karibu na eneo la kazi la baba yake kaskazini mwa Italia baada ya kutoweka mwezi Aprili 2021 na uchunguzi wa maiti ulionyesha shingo yake ilikuwa imevunjika na kutafsiriwa kuwa alinyongwa au kubanwa.


Mjomba wake, Danish Hasnain amehukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani, kwa kuhusika katika mauaji hayo huku baba wa Abbas akidai hana hatia juu ya mashitaka hayo na pia anataka kumjua muuaji wa binti yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad