Askofu Tanzania Amkosoa Vikali Papa Francis 'Kheri nibariki jiwe sio ushoga, usagaji...'




Askofu wa Jimbo Katoliki Geita Flavian Kassala amesema hayuko tayari kubariki ndoa zilizo kinyume na maadili kwani ni kinyume na maagano ya Mungu ya kutaka Binadamu wakazaliane na kuendeleza vizazi ulimwenguni

Askofu Kassala amesema bora abariki jiwe ukajengee nyumba na sio kubariki mambo yaliyo kinyume na maadili

Akihubiri katika Misa ya Kitaifa ya Krisimasi amesema ndoa zisizo na maadili ni kwenda kinyume na maandiko ya Mungu yanayotaka wanadamu wakazaliane na kuendeleza vizazi

Aidha, amesema Binadamu anakataa uumbaji wa Mungu na kufanya mambo yaliyokatazwa huku wakitaka na kanisa liyabariki jambo ambalo amelipinga vikali

"Binadamu amemuacha Mungu na kufanya mambo yaliyokatazwa, Binadamu amekataa uumbaji na kuendeleza uumbaji na sasa wanafanya mambo machafu yasiyompendeza Mungu, wamekuwa wakiharibu vizazi kwa kutoa Mimba na sasa wanataka tubariki ndoa zisizo na maadili, kwangu bora nibariki jiwe lakini sio uchafu huo" -Askofu Kassala

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad