Bandari ya Dar yazidiwa mizigo

Bandari ya Dar yazidiwa mizigo


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Plasduce Mbossa amesema, mizigo inayoingia nchini kwa sasa kupitia bandari ya Dar es Salaam ni mingi ikilinganishwa na miundombinu iliyopo na mpaka sasa jumla ya meli 41 zipo kwenye lango la bandari zinasubiri foleni ya kushusha mizigo.

Amebainisha hayo katika kikao cha pamoja baina ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila na uongozi wa bandari kilichokuwa kikijadili namna bora ya kuondosha mizigo bandarini kwa wakati.

"Tunaendelea kupambana kuhakikisha mizigo inatoka bandarini haraka na kwa gharama nafuu, wastani kwa siku tunapokea meli tano mpaka saba na kupambana kuzitoa zote siku hiyohiyo tukishirikiana na bandari kavu, kwa sasa tuna neema ya kupokea meli nyingi sana kwenye bandari yetu lakini bado miundombinu ni ileile" Mbossa

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ameiomba TPA kutoa kipaumbele kwa mizigo inayokwenda kwenye masoko makubwa nchini kama Kariakoo hasa kwa msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kuwa mizigo mingi inayoingia katika bandari ya Dar es Salaam ndiyo inayosukuma serikali kutafuta wawekezaji wa kufanya maboresho na utanuzi wa miundombinu ya bandari hiyo.

Kupitia kikao hiko wamejadili namna ya kuongeza ufanisi, uondoshaji wa mizigo kwa gharama nafuu na kuweza kuhudumia nchi jirani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad