Bei ya Dizeli, Petroli yashuka




BEI ya mafuta kwa mwezi Disemba, imeshuka kutokana na kupungua kwa bei za mafuta ghafi kwenye soko la dunia, pamoja na  gharama za kuagiza nishati hiyo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dk.James Mwainyekule, bei ya mafuta ya petrol imepungua kwa asilimia 0.89, ikiwa ni wastani wa Sh. 116, huku upande wa dizeli yakishuka kwa asilimia 9.11, sawa na wastani wa Sh. 148, kwa kila lita.

Taarifa hiyo imeonesha viwango elekezi vya bei ya mafuta, ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, bei impungua kutoka Sh. 3,274 iliyokuwa Novemba hadi kufikia Sh. 3,158, inayoanza kutumika leo tarehe 6 Disemba mwaka huu.

Kwa upande wa bei ya mafuta ya taa, imebaki kama ilivyo.


“Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Desemba 2023 yanatokana na kupungua kwa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 8.72% na gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 27 kwa petroli na asilimia 23 kwa dizeli,” imesema taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad