Binti Mkosoaji wa Serikali ya Rwanda, Anne Rwigara Afariki Dunia Ghafla


Mkosoaji wa Serikali ya Rwanda, Anne Rwigara (41) amefariki Dunia ikielezwa ni baada ya kulalamikia maumivu ya tumbo kwa saa 8 yaliyopelekea Viungo vyake vya Mwilini kushindwa kufanya kazi

Anne ambaye alikuwa binti wa marehemu Mfanyabiashara maarufu nchini Rwanda, Assinapol Rwigara, amefariki akiwa Marekani alikokuwa akiishi huku Mama yake akisema kifo cha binti yake kilikuwa fumbo kwani hakuwa mgonjwa

Anne na mama yake, Adeline Rwigara walikaa gerezani kwa mwaka mmoja kwa tuhuma za kukwepa kulipa Kodi na Makosa ya Uchaguzi ambapo Mamlaka ya Mapato Rwanda ilisema familia ya Rwigara inadaiwa Dola Milioni 6.7 za kodi na hivyo Serikali ilifunga biashara ya familia na kufungia akaunti zao za benki

Anne pia ni Dada wa Diane Rwigara ambaye alishiriki Uchaguzi Mkuu mwaka 2017 akiwania Urais dhidi ya Paul Kagame. Mnamo Septemba 2017, Diane, Mama yake na Watu wengine wanne walishtakiwa kwa ‘kuchochea uasi’ kati ya makosa mengine, lakini wakaachiwa mnamo Desemba 2018
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad