Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa Wakuu wa Wilaya sita ambapo amemuhamisha Maveka Simon Maveka kutoka Wilaya va Chunya kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa na Remidius Mwema Emmanuel amehamishwa kutoka Wilaya ya
Kongwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto.
Amemuhamisha pia Mbaraka Alhaji Batenga kutoka Wilaya ya Kiteto kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya na Kanali Hamis Mayamba Maiga amehamishwa kutoka Wilaya ya Rombo kwenda kuwa Mkuu wa Wilava va Misenyi huku Kanali Wilson Christian Sakullo akihamishwa kutoka Wilaya ya Misenyi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro na Raymond Stephen Mwangwala amehamishwa kutoka Wilaya ya Ngorongoro kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo.
Katika hatua nyingine Rais Samia amefanya uhamisho wa Wakurugenzi wa Halmashauri 15 ambapo amemuhamisha Rose Robert Manumba kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Rehema Said Bwasi amehamishwa kutoka Malinyi kwenda kuwa Mkurugenzi Mendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
Yefred Edson Myenzi amehamishwa kutoka Mbulu kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita akichukua nafasi ya Zahara Muhiddin Michuzi ambaye amehamishiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Lena Martin Nkya amehamishwa kutoka Ifakara kwenda kuwa DED Tunduma na Chiriku Hams Chilumba amehamishwa kutoka Namtumbo kwenda kuwa Mkurugenzi DED Kigoma, Kisena Magena Mabuba amehamishwa kutoka Kilosa kwenda kuwa DED Shinyanga akichukua nafasi ya Simon Sales Berege ambaye anakwenda kuwa DED Rufiji akichukua nafasi ya Michael John Gwimile ambaye anakwenda kuwa DED Kilosa.
Wengine ni Regina Lazaro Bieda ambaye amehamishwa kutoka Momba kwenda kuwa DED
Kibaha, Mwajuma Abasy Nasombe amehamishwa kutoka Mwanga kwenda kuwa DED Moshi na Rashid Karim Gembe amehamishwa kutoka Moshi kwenda kuwa DED Mkinga.
Zahara Abdul Msangi amehamishwa kutoka Mkinga kwenda kuwa DED Mwanga na Philemon Mwita Magesa amehamishwa kutoka Tunduma kwenda kuwa DED Namtumbo na Butamo Nuru Ndalahwa amehamishwa kutoka Halmashauri ya
Wilaya ya Kibaha kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba.