BREAKING : Vifo Vyafika 47 Mafuriko Hanang Katesh


Mafuriko Hanang Katesh
Mafuriko Hanang Katesh

BREAKING: Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema hadi kufikia leo saa kumi jioni idadi ya vifo kutokana na mafuriko Wilayani Hanang imeongezeka na kufikia Watu 47 huku waliojeruhiwa wakifikia 85 na wengine wakihofiwa kufukiwa na tope baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha Wilayani humo.

RC Sendiga amesema eneo kubwa lililoathiriwa na mafuriko hayo ni kata ya Gendabi na katikati ya Mji wa Katesh ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya ya Hanang ambako nyumba za Watu zimezingirwa na mafuriko na miti iliyosombwa na mafuriko kutoka sehemu ya Mlima Hanang kulikosababisha barabara ya Katesh kwenda Singida katika eneo la Mjini Katesh kushindwa kupitika kwa muda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad