Mahakama Kuu imetengua uamuzi wa Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililoidhinisha uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho uliowavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18
Jaji Cyprian Mkeha amesema kitendo cha wajumbe wa Kamati Kuu kuwa wajumbe wa Baraza Kuu na kutoa uamuzi wa Rufaa ni kinyume cha Kanuni za Haki Asili. Pia, Mahakama imeamuru #CHADEMA kuzingatia Haki wakati ikishughulikia rufaa za Wanachama hao
Mdee na wenzake 18 walifungua kesi Mahakamani kupinga uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA uliotolewa Mei 11, 2022 na kutupilia mbali Rufaa walizokata kuipinga Kamati Kuu