Dawa za Kulevya KILO 3182 Zadakwa Dar es Salaam na Iringa

Dawa za Kulevya

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Tanzania (DCEA) imekamata kilogramu 3182 za dawa za kulevya aina ya heroin na methamphetamine katika operesheni maalum iliyofanyika Jijini Dar es Salaam na Iringa kati ya tarehe 5 hadi 23 mwezi December, 2023 ambapo Watu saba wamekamatwa kuhusika na dawa hizo na wawili kati yao wana asili ya Asia.


Akiongea Jijini Dar es salaam leo December 27,2023, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo amesema “Kiasi hiki cha dawa za kulevya kinajumuisha kilogramu 2,180.29 za dawa aina ya methamphetamine a kilogramu 1001.71 aina ya heroin zilizokamatwa katika Wilaya za Kigamboni, Ubungo na Kinondoni jijini Dares Salaam pamoja na Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa”


“Ukamataji huu umehusisha kiasi kikubwa cha dawa za kulevya ambacho hakijawahi kukamatwa katika historia ya Tanzania tangu kuanza kwa shughuli za udhibiti wa dawa za kulevya, hivyo Watuhumiwa waliokamatwa ni miongoni mwa mitandao mikubwa ya wauzaji wa dawa za kulevya inayofuatiliwa nchini na duniani.


“Aidha, dawa hizi zilizozikamata zilikuwa zimefungashwa kwenye vifungashio vya bidhaa zenye chapa mbalimbali za kahawa na majani ya chai, mbinu hii inatumika kwa lengo la kurahisisha usafirishaji wake na kukwepa kubainika”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad