Diamond amuonya mwanaume anayemnyemelea Zuchu

 

Zuchu

Staa wa bongo kutoka Tanzania Diamond Platnumz alijitokeza kudhihirisha mapenzi yake kwa Zuchu baada ya mwanamume kuanza kumtaka watoke kimapenzi.


Mwimbaji huyo wa Bongo aliamua kumuweka wazi mwanamume aliyekuwa akimmezea Zuchu mate huku akimuonya kuwa aachane na mwanamke wake.


Diamond aliingia kwenye mitandao ya kijamii na kusambaza picha ya skrini iliyonasa maandishi ya kimapenzi ambayo mwanaume huyo alimtumia Zuchu.


“Nipigie simu ukiwa tayari..” Moja ya SMS ilisomwa.


"Nashida ya kuonana na wewe leo kwa 10min, utaniambia kama kuna gharama zozote za kukuona," mtu huyo anamwambia Zuchu katika ujumbe mwingine.


Akijibu meseji hizo, Diamond alimtahadharisha mwanamume huyo kuwa anafahamu kuwa anamtongoza mwanamke wake kwani Zuchu ndiye aliyemripoti.


“Mwenye hii namba, nikujuze tu kuwa mwanamke wangu @officialzuchu amenifikishia habari zako!” Diamond aliandika.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad