Dkt. Mpango 'Sitakufa mpaka nitakapokamilisha kazi ya Mungu'

Dkt. Mpango 'Sitakufa mpaka nitakapokamilisha kazi ya Mungu'

Dkt. Mpango 'Sitakufa mpaka nitakapokamilisha kazi ya Mungu'

Makamu wa Rais, Dkt Phillip Mpango, leo asubuhi amesali kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Kiwanja cha Ndege, jijini Dodoma, akionekana na bashasha na afya njema.


"Yamesemwa mengi na wengine bado wanasema mimi ni mzuka, wale mnaopenda kusoma biblia Zaburi ya 100:18 aya ya 17 inasema sitakufa nitaishi...... kwahiyo mkae na amani niko salama nilikwenda nje kufanya shughuli maalumu kwa takribani mwezi mmoja sijapungua hata kidogo"


"Mitandao ni mizuri lakini baadhi ya watu wanaitumia visivyo, mkiandika uongo mnawaumiza watu wengi, wapo watu wengi ambao wameumizwa na maneno yasio ya msingi, tujitahidi sana kutumia mitandao ipasavyo kwa kumuogopa Mungu, wale waliokuwa wanatuma picha yangu na mshumaa pembeni, wengine wakasema mzee amekata moto"


"Mimi kufa bado kabisa, kazi ambayo Mungu alinituma kufanya sijaimaliza, wakati utakapofika nitarejea kwa muumba wangu, asanteni sana najua mmeniombea kweli," amesema Dkt. Philip Mpango baada ya kushiriki ibada ya Jumapili katika kanisani katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska kiwanja cha ndege Dodoma leo Disemba 10, 2023.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad