"Tatizo la Chama na Simba ni ushahidi halisi wa namna Simba walivyokosea katika madirisha mengi ya usajili kwa miaka mitatu iliyopita....hawakuwahi kuondoa umuhimu wake uliopitiliza klabuni. Alipokuwepo hapo awali,, alipokwenda Morocco, na aliporudi nyayo zake zilisimama juu ya utosi wa Simba. Mwanzoni tu mwa msimu alienda mazoezini, alipoona hakuna maajabu akagoma kwenda Uturuki. Ameichukua klabu mateka kwa muda mrefu."